Sunday, February 21, 2016

Paul Makonda Na Meya Wa Kinondoni ( Chadema ) ' Washikana Mashati ' Kuhusu Mipaka Ya Kiutendaji

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob na Mkuu wa wilaya hiyo, Paul Makonda wameingia kwenye mvutano kuhusu kuvuka mipaka ya utendaji wa halmashauri hiyo.

Saturday, February 20, 2016

Kutana na huyu Mtangazaji wa TV Nigeria aliyemsifia Rais Magufuli kwa dakika 9

Tuliyaona Magazeti mbalimbali ya Uarabuni, Australia, South Africa na nchi nyingine kadhaa yakisifia utendaji kazi wa raisi mpya wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli na sasa ni zamu ya huyu mtangazaji wa TV nchini Nigeria anaesema kwanini Rais Magufuli ni raisi bora wa Afrika kwa sasa.

Chuchu Hans amtetea Ray, Asema hajichubui bali ni maisha yamemkubali

Baada ya kuandamwa na baadhi ya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kuhusu weupe wake, Ray Kigosi amesema kwamba yeye hajawahi kujichubua bali huwa anakunywa maji mengi pamoja na kufanya mazoezi.

Nay "Sikusema kuwa Wema hana ujauzito" ajitetea baada ya mshabiki kumshambulia

Nay wa Mitego amesema mashabiki wamemcharukia kuwa ana mdomo mbaya baada ya taarifa kuwa huenda mimba ya Wema Sepetu imetoka kulingana na post ya mpenzi wake Idriss sultan.

Huddah Monroe ajitangaza kwasasa kuwa yeye ni tajiri

Mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe, amejitapa na utajiri alionao kwa sasa na kusema kwamba uji wa chumvi aliwahi kunywa mara moja katika kumbukumbu za maisha yake.

Rwanda Wampongeza Rais Magufuli Kwa Kutumbua MAJIPU Bandarini.

WAFANYABIASHARA wa Rwanda wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Rais John Magufuli katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa kuimarisha ufanisi wa bandari, kukuza biashara baina ya Tanzania na nchi jirani.

Huyu Ndo Binti Aliyeongoza Kitaifa Katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato Cha Nne

Huyu ndiye Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza  Kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha Nne  toka  shule  ya  Canossa Girls.Anaitwa Butogwa Charles Shija, akiwa mwenye furaha, nyumbani kwa wazazi wake Kipunguni Jijini la Dar es Salaam jana. 

Paul Scholes mapenzi yake kwa Man United yanataka kumuachisha kazi BT Sport ili …

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Man United na timu ya taifa ya Uingereza Paul Scholes ambaye amewahi kuichezea klabu ya Man United kwa zaidi ya miaka 15, anatajwa kutaka kuacha kazi yake ya uchambuzi wa soka katika kituo cha BT Sport kwa ajili ya mapenzi yake kwa Man United.

Friday, February 19, 2016

Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Uganda: Museveni Anaongoza kwa Asilimia 62.03


Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi nchini Uganda yanaonesha kuwa Rais Yoweri Museveni kwa tiketi ya NRM anaongoza akiwa na zaidi ya kura milioni 1.3 sawa na asilimia 62.03.

U Heard ya leo imemgusa Shilole, ukweli kuhusu mahusiano yake mapya baada ya kuachana na Nuh Mziwanda? …(+AUDIO)

Kwenye U Heard ya Clouds fm leo ni kuhusu mrembo Shilole ambaye tangu kuachana na mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda haijafahamika wazi ni nani mwingine amechukua nafasi, Sasa leo Soudy Broun kamvutia waya na kuhoji kuhusu ukaribu wake na Nedy Music.
Full stori ipo kwenye hii sauti hapa chini….

Mvuto wa ramani za viwanja 12 vitakavyotumika Kombe la Dunia 2022 Qatar (+Pichaz)


Kwa kawaida maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia hufanyika miaka zaidi ya minne kabla ya nchi husika kuanza kupokea timu katika miji yao. Imekuwa kawaida kwa kila nchi inayotarajia kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia kutengeneza viwanja vipya na vyenye hadhi kwa ajili ya michuano hiyo.

Mambo Manne Yaliyochangia Anguko la Shule za Vipaji Katika Matokeo Ya Mtihani wa Kidato cha Nne


Anguko la shule za sekondari za Serikali zikiwamo za vipaji maalumu katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, limedaiwa kusababishwa na walimu kukata tamaa, miundombinu duni na mazingira magumu ya kufundishia na kusomea.

Breaking News: Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka....Yatazame Hapa


Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
back to top