
Akizungumza katika kipindi cha eNewz cha East Africa Television, Ray alisema kwamba huwa anakwenda saluni mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake 'Scrub' ili akiwa anafanya kazi zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake.
Muigizaji huyo aliyeachia filamu ya ‘Tajiri Mfupi’ hivi karibuni, alisema hajawai tumia mkorogo kama baadhi ya watu wanavyodai.
Naye mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba mpenzi wake hajichubui bali ni maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua sanaa na kipaji chake.
0 comments:
Post a Comment